Al-Ankaboot 29:41
العنكبوتمَثَلُ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَوْلِيَآءَ كَمَثَلِ ٱلْعَنكَبُوتِ ٱتَّخَذَتْ بَيْتًا ۖ وَإِنَّ أَوْهَنَ ٱلْبُيُوتِ لَبَيْتُ ٱلْعَنكَبُوتِ ۖ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ
Mfano wa wale waliowafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyojitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mfano wa wale waliowafanya masanamu ni wategemewa badala ya Allah Mtukufu, wakawa wanatarajia msaada wao, ni kama mfano wa buibui aliyejitengenezea nyumba ili imuhifadhi, isimfae kitu alipokuwa na haja nayo. Hivyo basi ndivyo walivyo hawa washirikina, hawakuwafaa kitu wale waliowachukuwa kuwa ni wasaidizi wao badala ya Allah Mtukufu. Na kwa hakika, nyumba iliyo dhaifu zaidi ni nyumba ya buibui, na lau wao wangekua wakilijua hilo wasingewafanya wao ni wasaidizi wenye kutegemewa badala ya Allah Mtukufu, kwani wao hawawanufaishi wala hawawadhuru.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net