Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 40

Al-Ankaboot 29:40

العنكبوت

فَكُلًّا أَخَذْنَا بِذَنۢبِهِۦ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِ حَاصِبًا وَمِنْهُم مَّنْ أَخَذَتْهُ ٱلصَّيْحَةُ وَمِنْهُم مَّنْ خَسَفْنَا بِهِ ٱلْأَرْضَ وَمِنْهُم مَّنْ أَغْرَقْنَا ۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ

Maana

Basi kila mmoja tulimtesa kwa mujibu wa makosa yake. Kati yao wapo tuliowapelekea kimbunga cha changarawe; na kati yao wapo walionyakuliwa na ukelele; na kati yao wapo ambao tuliwadidimiza katika ardhi; na kati yao wapo tuliowazamisha. Wala Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wenyewe wakijidhulumu nafsi zao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi kila mmoja tulimtesa kwa mujibu wa makosa yake. Kati yao wapo tulio wapelekea kimbunga cha changarawe; na kati yao wapo walio nyakuliwa na ukelele; na kati yao wapo ambao tulio wadidimiza katika ardhi; na kati yao wapo tulio wazamisha. Wala Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wenyewe wakijidhulumu nafsi zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kila mmoja, kati ya hao waliotajwa, tulimkamata kwa dhambi zake: kati yao kuna wale tuliyowatumia mawe ya udongo ulioshikana, nao ni watu wa Lûṭ, na kati yao kuna waliopatwa na ukelele, nao ni watu wa Ṣāliḥ na watu wa Shu‛ayb, na kati yao kuna tuliowadidimiza ardhini kama vile Qārūn, na katika wao kuna tuliowazamisha majini, nao ni watu wa Nûḥ na Fir‛awn na jamaa zake. Na Allah Mtukufu hakuwa ni Mwenye kuwaangamiza hawa kwa dhambi za wengine akawa ni mwenye kuwadhulumu kwa kuwaangamiza wao bila kustahili, lakini wao walikuwa wakijidhulumu wenyewe kwa kujistarehesha kwa neema za Mola wao na kumuabudu asiyekuwa Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net