Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 42

Al-Ankaboot 29:42

العنكبوت

إِنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ مِن شَىْءٍ ۚ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ

Maana

Kwa hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu wanachokiomba badala yake Yeye. Na Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu wanacho kiomba badala yake Yeye. Na Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye hikima.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu Anavijua vile wanavyomfananisha navyo washirikina na kumshirikisha navyo, na kwamba hivyo, kwa hakika, si kitu chochote, bali ni majina tu waliyoyaita, havinufaishi wala havidhuru. Na Yeye Ndiye Mshindi Mwenye uwezo wa kuwatesa waliomkufuru, Ndiye Mwenye hekima katika uendeshaji mambo Wake na utengenezaji Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net