Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 86

Al-Qasas 28:86

القصص

وَمَا كُنتَ تَرْجُوٓا۟ أَن يُلْقَىٰٓ إِلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبُ إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ ظَهِيرًا لِّلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Nawe hukuwa unataraji kuletewa Kitabu; lakini ni rehema tu ya Mola wako Mlezi. Basi kamwe usiwe msaidizi wa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nawe hukuwa unataraji kuletewa Kitabu; lakini ni rehema tu ya Mola wako Mlezi. Basi usiwe msaidizi wa makafiri. [86]

[86] Ewe Mtume! Wewe hukuwa wewe ukitaraji na ukingojea uteremshiwe hii Qur'ani. Lakini Mwenyezi Mungu amekuteremshia kutoka kwake kwa kukurehemu wewe na umma wako. Basi ikumbuke neema hii, na shikilia kuifikisha. Wala usiwe wewe na wanao kufuata kuwa wasaidizi wa makafiri kwa wanayo yataka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hukuwa ukitarajia, ewe Mtume, kuteremkiwa na Qur’ani, lakini Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Alikurehemu Akakuteremshia. Basi mshukuru Allah Mtukufu Aliyetukuka kwa neema Zake, na usiwe ni mwenye kuwasaidia watu wa ushirikina na upotevu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net