Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 85

Al-Qasas 28:85

القصص

إِنَّ ٱلَّذِى فَرَضَ عَلَيْكَ ٱلْقُرْءَانَ لَرَآدُّكَ إِلَىٰ مَعَادٍ ۚ قُل رَّبِّىٓ أَعْلَمُ مَن جَآءَ بِٱلْهُدَىٰ وَمَنْ هُوَ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ

Maana

Hakika yule aliyekulazimisha kuifuata Qur-ani, hapana shaka atakurudisha pahala pa marejeo. Sema, "Mola wangu Mlezi ndiye anayemjua zaidi mwenye kuja na uongofu, na ni nani aliyemo katika upotovu ulio dhahiri."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika aliye kulazimisha kuifuata Qur'ani hapana shaka atakurudisha pahala pa marejeo. Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuja na uwongofu, na nani aliyomo katika upotofu ulio dhaahiri. [85]

[85] Hakika Mwenyezi Mungu aliye kuteremshia Qur'ani na akakulazimisha uifikishe kwa watu na ushikane nayo hapana shaka atakurudisha kwenye miadi, nako ni Siku ya Kiyama, ili apambanue baina yako na wale wanao kukadhibisha. Ewe Mtume! Waambie makafiri: Mola wangu Mlezi ndiye anaye jua kwa ujuzi usio pikuliwa na yeyote, nani aliye mpa uwongofu na uwongozi, na nani aliye tumbukia katika upotovu unao tambulikana na kila mwenye akili nzima.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Yule Aliyekuteremshia wewe, Qur’ani, ewe Mtume, na akakulazimisha wewe uifikishe na ushikamane nayo, ni Mwenye kukurudisha kule ulikotoka, nako ni Makkah. Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Mola wangu Anamjua zaidi yule aliyeleta uongofu na yule ambaye ameenda nje ya haki waziwazi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net