Al-Qasas 28:84
القصصمَن جَآءَ بِٱلْحَسَنَةِ فَلَهُۥ خَيْرٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن جَآءَ بِٱلسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَى ٱلَّذِينَ عَمِلُوا۟ ٱلسَّيِّـَٔاتِ إِلَّا مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Atakayetenda mazuri, atapata malipo bora kuliko hayo mazuri aliyoyatenda. Na atakayetenda mabaya, hawalipwi watendao mabaya isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Atakaye tenda wema atapata malipo bora kuliko huo wema alio utenda. Na atakaye tenda uovu, hawalipwi watendao uovu ila waliyo kuwa wakiyatenda. [84]
[84] Mwenye kuja na wema, nao ni Imani na vitendo vyema, atapata malipo marudufu kwa ajili yake. Na mwenye kuja na uovu, nao ni ukafiri na maasi, halipwi ila mfano wa vitendo vyake viovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mwenye kuja, Siku ya Kiyama, na utakasaji wa Allah Mtukufu Mmoja na matendo mema yanayolingana na Sheria ya Allah Mtukufu, basi yeye atakuwa na malipo makubwa yenye kheri zaidi kuliko kile alichokifanya. Na kheri hiyo ni Pepo na starehe ya daima. Na mwenye kuja na matendo mabaya, hawatalipwa hao waliofanya maovu kwa matendo yao, isipokuwa yale waliokuwa wakiyafanya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net