Al-Qasas 28:83
القصصتِلْكَ ٱلدَّارُ ٱلْـَٔاخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا ۚ وَٱلْعَـٰقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ
Hayo ndiyo makazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasiotaka kujiinua juu katika dunia wala uharibifu. Na mwisho mwema ni wa wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hayo ndiyo makaazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasio taka kujitukuza duniani wala ufisadi. Na mwisho mwema ni wa wachamngu. [83]
[83] Hayo ndio makaazi ambayo umesikia khabari zake, ewe Mtume, na zikakufikia sifa zake, nayo ni Pepo. Tumeiweka makhsusi kwa ajili ya Waumini wat'iifu, wasio taka kujipa ubora na utukufu wa kidunia, na wala hawapotoki kuendea ufisadi na maasi. Na mwisho mwema ni wa wale ambao nyoyo zao zimejaa khofu ya Mwenyezi Mungu, na wanatenda yanayo mridhisha Yeye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hiyo ndiyo Nyumba ya Akhera. Tumewapatia, ile starehe yake, wale ambao hawataki kuifanyia kiburi haki hapa duniani wala kufanya uharibifu humo. Na mwisho wenye kushukuriwa, nayo ni pepo, ni wa yule aliyejikinga na adhabu ya Allah Mtukufu na akafanya mema na akaacha mambo yaliyoharamishwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net