Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 82

Al-Qasas 28:82

القصص

وَأَصْبَحَ ٱلَّذِينَ تَمَنَّوْا۟ مَكَانَهُۥ بِٱلْأَمْسِ يَقُولُونَ وَيْكَأَنَّ ٱللَّهَ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ وَيَقْدِرُ ۖ لَوْلَآ أَن مَّنَّ ٱللَّهُ عَلَيْنَا لَخَسَفَ بِنَا ۖ وَيْكَأَنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلْكَـٰفِرُونَ

Maana

Na wale waliotamani kuwa pahala pake jana, wakawa wanasema, "Kumbe Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humkunjia amtakaye. Ingelikuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani, angelitudidimiza. Kumbe makafiri hawafanikiwi!"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale walio tamani kuwa pahala pake jana, wakawa wanasema: Kumbe Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humdhikisha amtakaye. Ingeli kuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani angeli tudidimiza. Kumbe makafiri hawafanikiwi! [82]

[82] Na wale walio kuwa karibuni wakikitamani cheo chake cha duniani, wakawa wanatamka maneno ya masikitiko na majuto baada ya kuyafikiri yaliyo msibu yeye. Wakawa wanasema: Hakika Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake Waumini na wasio kuwa Waumini. Na humdhikisha amtakaye katika hao. Na wakawa wanasema kwa kushukuru: Lau kuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani kwa kutupa uwongofu tukafuata Imani, na akatuhifadhi tusiporonyoke angeli tutia katika mitihani kwa kutukubalia tuliyo kuwa tunayatamani, na akatufanyia kama alivyo mfanyia Qaruni. Hakika wanao ipinga neema ya Mwenyezi Mungu hawafanikiwi kwa kuokoka na adhabu yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliotamani kuwa kama yeye jana yake wakawa wanasema, wakiwa na uchungu, wenye kuzingatia na wenye kuiogopa adhabu isiwashukie, Hakika Allah Mtukufu Anamkunjulia riziki Anayemtaka miongoni mwa waja Wake, na Anambania Anayemtaka miongoni mwao. Lau si Allah Mtukufu kutuneemesha kwa kutotuadhibu kwa tulilolisema, Angetudidimiza sisi ardhini kama Alivyomfanya qarûn. Kwani hujui kwamba makafiri hawafaulu, hapa duniani wala Akhera?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net