Al-Qasas
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَأَصْبَحَ ٱلَّذِينَ تَمَنَّوْا۟ مَكَانَهُۥ بِٱلْأَمْسِ يَقُولُونَ وَيْكَأَنَّ ٱللَّهَ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ وَيَقْدِرُ ۖ لَوْلَآ أَن مَّنَّ ٱللَّهُ عَلَيْنَا لَخَسَفَ بِنَا ۖ وَيْكَأَنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلْكَـٰفِرُونَ 82
{82} "Na wale waliotamani kuwa pahala pake jana;" yaani, wale wanaotaka maisha ya ulimwengu huu, ambao walisema: Laiti tungekuwa na mfano wa kile alichopewa Qarun, "wakawa wanasema" wakiwa na hofu na wasiwasi na kuogopa adhabu kutokea kwao: "Kumbe Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humkunjia amtakaye." Yaani, Yeye hupunguza riziki kwa amtakaye. Tulijua basi kwamba kupewa kwake Qarun sio ushahidi wa kheri ndani yake, na kwamba tulikuwa tumekosea kwa kusema: Yeye ni mtu wa bahati kubwa. Na "Ingelikuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani," basi hakutuadhibu kwa kile tulichosema; lau si fadhila yake na neema yake; "angelitudidimiza." Kwa hivyo kuangamizwa kwa Qarun ikawa adhabu kwake na mfano na mawaidha kwa wengine, ili wale waliomkamata wasikie jinsi walivyotubu, na mawazo yao ya kwanza yalibadilika. "Kumbe makafiri hawafanikiwi" katika ulimwengu huu wala katika Akhera.