Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 81

Al-Qasas 28:81

القصص

فَخَسَفْنَا بِهِۦ وَبِدَارِهِ ٱلْأَرْضَ فَمَا كَانَ لَهُۥ مِن فِئَةٍ يَنصُرُونَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلْمُنتَصِرِينَ

Maana

Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kando na Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanaojinusuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanao jitetea. [81]

[81] Mwenyezi Mungu akamdidimiza katika ardhi, na ardhi ikammeza yeye na nyumba yake na vyote vilio kuwemo ndani yake, mali na mapambo yake. Hakuwa na wasaidizi wa kumkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na wala yeye mwenyewe hakuweza kujinusuru nafsi yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi tukamdidimiza Qārūn pamoja na nyumba yake ndani ya ardhi. Na hakuwa na askari wa kumuokoa badala ya Allah Mtukufu, na hakuwa ni mwenye kujikinga na Allah Mtukufu yalipomshukia mateso Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net