Al-Qasas 28:80
القصصوَقَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ ٱللَّهِ خَيْرٌ لِّمَنْ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَـٰلِحًا وَلَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ٱلصَّـٰبِرُونَ
Na wakasema wale waliopewa elimu, "Ole wenu! Malipo ya Mwenyezi Mungu ni bora kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Wala hawatapewa hayo isipokuwa wenye subira."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakasema wale walio pewa ilimu: Ole wenu! Malipo ya Mwenyezi Mungu ni bora kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Wala hawatapewa hayo isipo kuwa wenye subira. [80]
[80] Ama wale ambao Mwenyezi Mungu amewaruzuku ilimu yenye manufaa hawakusalitika na hayo. Wakawaelekea walio danganyika kwa kuwanasihi wakiwaambia: Msiyatamani haya, wala msiiache Dini. Kwani yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ya thawabu na neema ni safi zaidi kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Na hiyo ni nasiha ya kweli ambayo hawaikubali ila wenye kuzipiga jihadi nafsi zao, na wakasubiri katika ut'iifu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wakasema, wale waliopewa elimu ya kumjua Allah Mtukufu na Sheria Yake na wakajua uhakika wa mambo, kuwaambia wale waliosema, «Tunatamani tuwe na mfano wa kile alichopatiwa Qārūn», Ole wenu! Muogopeni Allah Mtukufu na mumtii. Malipo mema ya Allah Mtukufu ni bora, kwa aliyemuamini Yeye na Mitume Wake na akafanya matendo mema, kuliko kile alichopatiwa Qārūn. Na haupokei ushauri huu na akaafikiwa kuufuata na kuufanyia kazi isipokua yule anayepigana jihadi na nafsi yake, anayevumilia katika kumtii Mola wake na anayejiepusha na mambo ya kumuasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net