Al-Qasas 28:79
القصصفَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِۦ فِى زِينَتِهِۦ ۖ قَالَ ٱلَّذِينَ يُرِيدُونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا يَـٰلَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَآ أُوتِىَ قَـٰرُونُ إِنَّهُۥ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ
Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale waliokuwa wanataka maisha ya duniani, "Laiti tungelikuwa tunayo kama aliyopewa Qaruni! Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale walio kuwa wanataka maisha ya duniani: Laiti tungeli kuwa tunayo kama aliyo pewa Qaruni! Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa. [79]
[79] Na Qaruni hakujali nasaha za watu wake. Akawatokea naye kajipamba mapambo yake. Wakadanganyika naye wale walio kuwa wanapenda starehe za maisha ya dunia, na wakatamani nao wangeli kuwa nayo mali na hadhi kubwa ya maisha kama aliyo pewa Qaruni
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi akatoka Qārūn akiwa kwenye pambo lake, akitaka kwa kufanya hivyo kuonyesha ukubwa wake na wingi wa mali yake. Na walipomuona wale wanaotaka pambo la uhai wa kilimwengu walisema, «Tunatamani lau sisi tungepatiwa mfano wa kile alichopatiwa Qārūn, cha mali, pambo na heshima. Kwa kweli, Qārūn ni mwenye sehemu kubwa ya dunia».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net