Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 78

Al-Qasas 28:78

القصص

قَالَ إِنَّمَآ أُوتِيتُهُۥ عَلَىٰ عِلْمٍ عِندِىٓ ۚ أَوَلَمْ يَعْلَمْ أَنَّ ٱللَّهَ قَدْ أَهْلَكَ مِن قَبْلِهِۦ مِنَ ٱلْقُرُونِ مَنْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُ قُوَّةً وَأَكْثَرُ جَمْعًا ۚ وَلَا يُسْـَٔلُ عَن ذُنُوبِهِمُ ٱلْمُجْرِمُونَ

Maana

Akasema, "Kwa hakika nimepewa haya kwa sababu ya elimu niliyo nayo." Je, hakujua kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha waangamiza, katika vizazi vya walio kabla yake, watu waliokuwa wenye nguvu zaidi kuliko yeye, na wenye makundi makubwa zaidi kuliko yake. Na wahalifu hawataulizwa habari ya dhambi zao."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Kwa hakika nimepewa haya kwa sababu ya ilimu niliyo nayo. Je! Hakujua kwamba Mwenyezi Mungu kesha waangamiza, katika vizazi vya walio kabla yake, watu walio kuwa wenye ngubvu zaidi kuliko yeye, na wenye makundi makubwa zaidi kuliko yake. Na wakosefu hawataulizwa khabari ya dhambi zao. [78]

[78] Basi Qaruni hakusikia nasaha ya watu wake, na akasahau fadhila ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yake. Na akajifanya hajui kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha waangamiza wengi walio mzidi yeye sana katika uwezo na mazoezi ya kuchuma mali kwa njia mbali mbali za uchumi. Na wakosefu hawaulizwi madhambi yao, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anayajua. Basi wataingizwa Motoni bila ya hisabu. Kuulizwa kwao ni kwa ajili ya kutahayarishwa tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Akasema Qārūn kuwaambia watu wake waliomuwaidhia, «Kwa hakika, mahazina haya ya mali nimeyapata kutokana na ujuzi na uwezo.»Kwani Qārūn hajui kwamba Allah Mtukufu ameshawaangamiza ummah wengi kabla yake waliokuwa na nguvu zaidi za kushinda na ukusanyaji zaidi wa mali? Na hawataulizwa wahalifu kuhusu dhambi zao, kwa kuwa Allah Mtukufu Anazijua, isipokuwa wataulizwa maulizo ya kuwalaumu na kuwasimanga. Na Atawatesa Allah Mtukufu kulingana na ujuzi Wake kuhusu wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net