Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 77

Al-Qasas 28:77

القصص

وَٱبْتَغِ فِيمَآ ءَاتَىٰكَ ٱللَّهُ ٱلدَّارَ ٱلْـَٔاخِرَةَ ۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ ٱلدُّنْيَا ۖ وَأَحْسِن كَمَآ أَحْسَنَ ٱللَّهُ إِلَيْكَ ۖ وَلَا تَبْغِ ٱلْفَسَادَ فِى ٱلْأَرْضِ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْمُفْسِدِينَ

Maana

Na utafute, kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu, makazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la duniani. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyokufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya uharibifu katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wafanyao uharibifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi. [77]

[77] Na katika utajiri na neema alizo kupa Mwenyezi Mungu toa fungu kwa ajili ya Njia ya Mwenyezi Mungu, na tenda a'mali kwa ajili ya makaazi ya Akhera. Na wala usiinyime nafsi yako fungu lake kwa matumizi ya halali katika dunia. Na wafanyie wema waja wa Mwenyezi Mungu, kama vile alivyo kufanyia wema wewe kwa neema zake. Wala usifanye uharibifu katika ardhi ukapita mipaka ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Subhanahu hawafurahii mafisadi kwa vitendo vyao viovu. Basi Qaruni hakusikia nasaha ya watu wake, na akasahau fadhila ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yake. Na akajifanya hajui kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha waangamiza wengi walio mzidi yeye sana katika uwezo na mazoezi ya kuchuma mali kwa njia mbali mbali za uchumi. Na wakosefu hawaulizwi madhambi yao, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anayajua. Basi wataingizwa Motoni bila ya hisabu. Kuulizwa kwao ni kwa ajili ya kutahayarishwa tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na utafute, kwa mali Aliyokupa Allah Mtukufu, malipo mema ya Nyumba ya Akhera, kwa kufanyia mambo ya kumtii Allah Mtukufu duniani, na usiache fungu lako la duniani la kustarehe humo kwa halali bila kupita kiasi, na uwafanyie watu hisani kwa kuwapa sadaka kama vile Allah Mtukufu Alivyokufanyia hisani kwa kukupa mali nyingi, na usitafute kile Alichokiharamisha Allah Mtukufu cha kuwadhulumu watu wako, kwani hakika Allah Mtukufu Hawapendi waharibifu, na Atawalipa kwa matendo yao mabaya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net