Al-Qasas 28:76
القصصإِنَّ قَـٰرُونَ كَانَ مِن قَوْمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيْهِمْ ۖ وَءَاتَيْنَـٰهُ مِنَ ٱلْكُنُوزِ مَآ إِنَّ مَفَاتِحَهُۥ لَتَنُوٓأُ بِٱلْعُصْبَةِ أُو۟لِى ٱلْقُوَّةِ إِذْ قَالَ لَهُۥ قَوْمُهُۥ لَا تَفْرَحْ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْفَرِحِينَ
Hakika Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhuluma. Na tulimpa hazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu kuzibeba. Watu wake walipomwambia, "Usijigambe! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaojigamba."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhulma. Na tulimpa khazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu kuzichukua. Walipo mwambia watu wake: Usijigambe! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanao jigamba. [76]
[76] Sura hii inasimulia kisa cha Qaruni. Naye alikuwa katika kaumu ya Musa. Akapanda kiburi juu yao kwa kughurika kwa nafsi yake na mali yake. Na Mwenyezi Mungu alikuwa kampa khazina za mali mengi. Hata ikawa funguo zake tu zikiwaemea kundi la wanaume wenye nguvu! Na alipo ghurika na neema ya Mwenyezi Mungu juu yake, na akakufuru kwa sababu yake, watu walimpa nasaha, wakamwambia: Usidanganyike kwa mali yako, wala furaha kwa ajili yake isikusaliti hata ukaacha kumshukuru Mwenyezi Mungu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu hawapendi watu walio danganyika na wakasalitika. Na funzo la kisa hichi ni kuwa makafiri walio mkataa Muhammad s.a.w. walighurika na mali yao. Basi Qur'ani inawaelezea kuwa mali yao si chochote cha kutajika ukilinganisha na mali ya Qaruni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Qārūn alikuwa ni miongoni mwa watu wa jamii ya Mûsã, rehema na amani zimshukie, akakiuka mpaka wake katika kuwa na kiburi na ujabari juu yao. Na tulimpa Qārūn mahazina mengi ya mali, mpaka ikafikia kiwango cha kuwa funguo zake zinawaelemea idadi kubwa ya watu wenye nguvu kuzibeba. Walipomuambia watu wake, «Usifanye kiburi ukawa na majivuno ya furaha kwa mali uliyonayo. Hakika Allah Mtukufu Hawapendi waja wake wenye kiburi ambao hawamshukuru Allah Mtukufu Aliyetukuka kwa kile Alichowapa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net