Al-Qasas 28:75
القصصوَنَزَعْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا فَقُلْنَا هَاتُوا۟ بُرْهَـٰنَكُمْ فَعَلِمُوٓا۟ أَنَّ ٱلْحَقَّ لِلَّهِ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ
Na tutatoa shahidi katika kila umma, na tutasema, "Leteni hoja zenu!" Hapo watajua kwamba hakika haki ni ya Mwenyezi Mungu, na yatawapotea yale waliyokuwa wakiyazua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tutatoa shahidi katika kila umma, na tutasema: Leteni hoja zenu! Hapo watajua kwamba hakika kweli ni ya Mwenyezi Mungu, na yatawapotea yale waliyo kuwa wakiyazua. [75]
[75] Na Siku ya Kiyama tutatoa kutoka kila umma shahidi, naye ndiye Nabii wao, wa kutoa ushahidi dhidi yao kwa waliyo kuwa wakiyafanya duniani. Hapo Sisi tutawaambia wakhalifu miongoni mwao: Nini hoja yenu kwa mliyo kuwa mkiyatenda ya ushirikina na maasi? Watashindwa kujibu, na watajua hapo kuwa Haki yote iko kwa Mwenyezi Mungu, tangu mwanzo mpaka mwisho. Na yatapotea, kama vinavyo potea vitu vilio potea, yote waliyo kuwa wakimzulia Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tutamtoa kwenye kila ummah, miongoni mwa ummah zenye kukanusha, shahidi, naye ni Nabii wao, atakayetoa ushahidi juu ya yaliyopita duniani ya ushirikina wao na ukanushaji wao Mitume wao. Tukaziambia ummah hizo zilizokanusha Mitume wake na yale waliyoyaleta kutoka kwa Allah Mtukufu, «Leteni hoja yenu juu ya kile mlichomshirikisha nacho Allah Mtukufu.» Wakati huo watajua kuwa hoja nzuri ni ya Allah Mtukufu juu yao, kuwa haki ni ya Allah Mtukufu, na kitawaondokea kile walichokuwa wakimzulia Mola wao, kisiwanufaishe hiko, bali kiwadhuru na kiwafikishe kwenye Moto wa Jahanamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net