Al-Qasas 28:74
القصصوَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَآءِىَ ٱلَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ
Na siku atakapowaita na akasema, "Wako wapi hao mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu?"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na siku atakapo waita na akasema: Wako wapi hao mlio kuwa mkidai kuwa ni washirika wangu? [74]
[74] Na pia, ewe Mtume, kumbuka siku watapo itwa washirikina na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wito wa kuwatahayarisha, wakaambiwa: Wako wapi washirika ambao mkidai kuwa ni miungu wa kukunusuruni, au waombezi wa kukuombeeni?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Siku ambayo Allah Mtukufu Atawaita hawa washirikina Awaambie, «Wako wapi washirika wangu ambao mlikuwa mkidai duniani kwamba wao ni washirika wangu?».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net