Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 73

Al-Qasas 28:73

القصص

وَمِن رَّحْمَتِهِۦ جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ لِتَسْكُنُوا۟ فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا۟ مِن فَضْلِهِۦ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Maana

Na ni katika rehema zake amewafanyia usiku na mchana ili mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ni katika rehema zake amekufanyieni usiku na mchana mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru. [73]

[73] Na miongoni mwa rehema za Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake ni kuwa kawaumbia usiku na mchana, inayo fuatana, ili wapate kupumzika usiku, na washughulikie kutafuta riziki zao na manufaa yao mengine wakati wa mchana, na watambue fadhila za Mwenyezi Mungu juu yao wapate kumshukuru. "Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya usiku umekukalieni moja kwa moja, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu atakaye kuleteeni mwangaza? Basi je, hamsikii? Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya mchana umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni usiku mkapumzika humo? Basi je, hamwoni? Na ni katika rehema zake amekufanyieni usiku na mchana mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru." Hapana shaka kuwa kuumbwa kwa dunia kwa namna yake ilivyo sasa na ilivyo wekwa kwa mnasaba wa jua, na kuzunguka kwake wenyewe kwa wenyewe kila siku, na kulizunguka jua kila mwaka, hapana shaka kwamba haya yanaonyesha dhaahiri uwezo wa Mwenyezi Mungu na upweke wake. Na Aya tukufu inawazindua watu watambue ukweli ambao yawapasa wauelewe, nao ni kwamba Yeye Mtukufu lau kuwa aliumba dunia iwe na usiku wa milele, au iwe na mchana wa milele, basi hapanapo mungu mwengine anaye weza kuwaneemesha watu kwa mchana na usiku wa kufuatana kama hivi. Na hivyo ni kuwa lau kuwa dunia inazunguka juu ya msumari-kati wake na pia kulizunguka jua kwa kiwango kimoja kiasi ya siku 365 takriban, yangeli tokea mabadiliko makubwa mno. Miongoni mwao ni kudumu giza katika nusu ya dunia, na kudumu mwangaza katika nusu ya pili takriban. Na kwa hivi joto lingeli panda katika nusu yenye mwangaza kwa kiasi kisicho weza kuchukulika. Na nusu yenye giza ingeganda kwa barafu. Na pande zote mbili zisingeweza kuchukua kitu chochote chenye uhai. Ama huu mpango ulivyo sasa unapelekea kupishana usiku na mchana, na kwa hivyo kunapatikana mapumziko na utulivu wakati wa usiku, na kushughulika wakati wa mchana. Na hali ya hewa inasilihi uhai wa binaadamu, na wanyama, na mimea. Na haya ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, ambazo zinapelekea tukubali uwezo wake, na tudumu kumshukuru.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa rehema Yake kwenu, enyi watu, ni kuwafanyia usiku na mchana Akatafautisha baina ya viwili hivi, Akaufanya huu usiku kuwa ni giza, ili mtulie humo na miili yenu ipumzike. Na Akawafanyia mchana kuwa ni mwangaza, ili mtafute maisha yenu na ili mumshukuru Yeye kwa kuwapa nyinyi neema zake hizo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net