Al-Qasas 28:72
القصصقُلْ أَرَءَيْتُمْ إِن جَعَلَ ٱللَّهُ عَلَيْكُمُ ٱلنَّهَارَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ ٱللَّهِ يَأْتِيكُم بِلَيْلٍ تَسْكُنُونَ فِيهِ ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeliufanya mchana umewakalia moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atayewaletea usiku mkapumzika humo? Basi je, hamwoni?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya mchana umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni usiku mkapumzika humo? Basi je, hamwoni? [72]
[72] Ewe Mtume! Waambie watu: Mwenyezi Mungu akikujaalieni mchana mfululizo bila ya usiku mpaka Siku ya Kiyama, yupo asiye kuwa Mwenyezi Mungu wa kukuleteeni usiku mkapata kupumzika na kazi za mchana? Hamna hayo nyinyi. Basi kwa nini hamzioni Ishara za Mwenyezi Mungu, mkaamini na mkaongoka?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie, «Nipeni habari iwapo Allah Mtukufu angewawekea mchana wa daima mpaka Siku ya Kiyama, ni mungu gani asiyekuwa Allah Mtukufu angewaletea usiku wa nyinyi kutulia na kupumzika ndani yake? Basi hamuoni kwa macho yenu kule kupishana kwa usiku na mchana?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net