Al-Qasas 28:71
القصصقُلْ أَرَءَيْتُمْ إِن جَعَلَ ٱللَّهُ عَلَيْكُمُ ٱلَّيْلَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ ٱللَّهِ يَأْتِيكُم بِضِيَآءٍ ۖ أَفَلَا تَسْمَعُونَ
Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeliufanya usiku umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea mwangaza? Basi je, hamsikii?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya usiku umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu atakaye kuleteeni mwangaza? Basi je, hamsikii? [71]
[71] Ewe Mtume! Sema: Enyi watu! Niambieni, Mwenyezi Mungu akikufanyieni usiku uendelee mfululizo bila ya mchana mpaka Siku ya Kiyama, je! Mnaye yeyote asiye kuwa Mwenyezi Mungu wa kukuleteeni mchana wenye mwangaza mkaweza kushughulikia maisha yenu na kuendesha mambo yenu ya dunia? Hamna hayo nyinyi. Basi kwa nini hamsikii kwa sikio la kuwaza na kuzingatia?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, «Nipeni habari, enyi watu, iwapo Allah Mtukufu angewawekea usiku wa daima mpaka Siku ya Kiyama, ni mungu gani asiyekuwa Allah Mtukufu angewaletea mwangaza wa nyinyi kupata kuona? Basi kwani nyinyi hamsikii kwa namna ya kufahamu na kukubali?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net