Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 87

Al-Qasas 28:87

القصص

وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنْ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ بَعْدَ إِذْ أُنزِلَتْ إِلَيْكَ ۖ وَٱدْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ

Maana

Wala kamwe wasikuzuie kuzifuata Aya za Mwenyezi Mungu baada ya kuteremshiwa wewe. Na lingania kwa Mola wako Mlezi, wala kamwe usiwe miongoni mwa washirikina.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala wasikuzuie kuzifuata Aya za Mwenyezi Mungu baada ya kuteremshiwa wewe. Na lingania kwa Mola wako Mlezi, wala usiwe miongoni mwa washirikina. [87]

[87] Wala makafiri wasikuachishe kuzifikisha Aya za Mwenyezi Mungu na kuzitenda, baada ya kwisha teremka wahyi (ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ukawa ndio Ujumbe wako. Na shikilia Wito kuwaitia watu kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu. Wala usiwe wewe wala wanao kufuata katika wasaidizi wa washirikina kwa kuwasaidia kwa wayatakayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wasikuzuiye wewe washirikina hawa na ufikishaji aya za Mola wako na hoja Zake baada ya kuwa Amekuteremshia kwako, na ufikishe ujumbe wa Mola wako, na usiwe ni miongoni mwa washirikina katika kitu chochote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net