Al-Qasas 28:88
القصصوَلَا تَدْعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ ۘ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ كُلُّ شَىْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُۥ ۚ لَهُ ٱلْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Wala usimwombe pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwinginewe. Hapana mungu isipokuwa Yeye. Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake. Hukumu ni yake, na kwake mtarejeshwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala usimwombe pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwenginewe. Hapana mungu ila Yeye. Kila kitu kitaangamia isipo kuwa Yeye. Hukumu iko kwake, na kwake mtarejezwa. [88]
[88] Wala usimwabudu mungu yeyote isipo kuwa Mwenyezi Mungu tu. Kwani hapana kabisa mungu wa kuabudiwa kwa haki isipo kuwa Yeye. Kila kitu isipo kuwa Mwenyezi Mungu kitaangamia na kwisha. Wa kudumu milele ni Yeye Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye mwenye hukumu ya kutekeleza duniani na Akhera. Na kwake Yeye ndiyo yako marejeo ya viumbe vyote, hapana hivi wala hivi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala usiabudu, pamoja na Allah Mtukufu, muabudiwa mwingine. Hapana muabudiwa kwa haki isipokuwa Allah Mtukufu. Kila kitu ni chenye kuangamia na kutoweka isipokuwa uso Wake. Uamuzi ni Wake. Na Kwake Yeye mtarudishwa baada ya kufa kwenu ili mhesabiwe na mlipwe. Katika aya hii kuna kuthibitisha sifa ya uso wa Allah Mtukufu, aliyetukuka, kama inavyonasibiana na ukamilifu Wake, ukubwa Wake na utukufu Wake.`
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net