Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 73

Al-Furqaan 25:73

الفرقان

وَٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّهِمْ لَمْ يَخِرُّوا۟ عَلَيْهَا صُمًّا وَعُمْيَانًا

Maana

Na wale ambao wanapokumbushwa Ishara za Mola wao Mlezi hawajifanyi viziwi nazo, na vipofu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale ambao wanapo kumbushwa Ishara za Mola wao Mlezi hawajifanyi viziwi nazo, na vipofu. [73]

[73] Na katika sifa zao ni kuwa mwenye kuwaidhi akiwapa mawaidha, na akawasomea Aya za Mwenyezi Mungu, humwelekea kumsikiliza, na nyoyo zao zikawaidhika, na macho yao hufunuka. Wala hawawi kama wale ambao wanatapatapa wanapo yasikia, wanapuuza, masikio yao hayapenyi kitu, wala macho yao hayafumbuki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ambao wakipewa mawaidha kwa aya za Qur’ani na dalili za upweke wa Allah Mtukufu hawajighafilishi nazo wakawa kama ambao ni viziwi hawakuzisikia na vipofu hawakuziona, lakini nyoyo zao zinazielewa na akili zao zinafunguka kuzikubali, na basi hapo wanajiporomosha kwa Allah Mtukufu hali ya kusujudu na kutii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net