Al-Furqaan
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّهِمْ لَمْ يَخِرُّوا۟ عَلَيْهَا صُمًّا وَعُمْيَانًا 73
{73} "Na wale ambao wanapokumbushwa Ishara za Mola wao Mlezi" ambazo aliwaamuru wazisikilize na kuongoka kwazo, "hawajifanyi viziwi nazo, na vipofu." Yaani, hawakabiliani nazo kwa kuzipa mgongo, na kujifanya viziwi wasizisikie, na kutoziangalia na kuzitia mioyoni kama vile wanavyofanya ambao hawakuziamini na kuzisadiki. Lakini hali yao kuhusiana nazo na wanapozisikia ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Hakika wanaoziamini Aya zetu ni hao tu ambao wakikumbushwa hizo, basi wao huanguka kusujudu, na humsabihi Mola wao Mlezi kwa kumhimidi, nao hawajivuni." Wanakabiliana nazo kwa kuzikubali, na kuzihitaji, na kujisalimisha kwazo, na wana masikio yanayosikia na mioyo inayofahamu, kwa hivyo wanaongezeka imani kwazo, na inakamilika kwazo yakini yao, na zinawaletea utanashati, na wanazifurahia furaha kubwa mno.