Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 74

Al-Furqaan 25:74

الفرقان

وَٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَٰجِنَا وَذُرِّيَّـٰتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَٱجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا

Maana

Na wale wanaosema: "Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wana wetu yaburudishayo macho, na utujalie tuwe waongozi kwa wacha Mungu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamngu. [74]

[74] Na wao humwomba Mola wao Mlezi awajaalie wake zao na watoto wao wawe wa kuwapoza moyo kwa vitendo vya kheri, na awajaalie wawe ni waongozi katika kheri ili watu wema wawafuate.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ambao wanamuomba Allah Mtukufu Aliyetukuka wakisema, «Mola wetu! Tutunukie miongoni mwa wake zetu na watoto wetu cha kutuliza macho yetu na chenye maliwazo na furaha kwetu, na utufanye ni kiigizo chema kwa wachamungu kutuiga».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net