Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 72

Al-Furqaan 25:72

الفرقان

وَٱلَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ ٱلزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا۟ بِٱللَّغْوِ مَرُّوا۟ كِرَامًا

Maana

Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uongo, na pindi wapitapo penye upuuzi, hupita kwa heshima yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uwongo, na pindi wapitapo penye upuuzi, hupita kwa hishima yao. [72]

[72] Na katika khulka za waja wa Mwingi wa Rehema ni kuwa wanajiepusha na kutoa ushahidi wa uwongo, na wakisadifu kukutana na mtu asiye kuwa na kauli au kitendo chema hawashirikiani naye katika hayo, na huacha kufuatana naye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ambao hawatoi ushahidi wa urongo wala hawahudhurii vikao vyake, na wapitapo kwa watu wa ubatilifu na ulaghai bila ya kukusudia wanapita hali ya kupa mgongo na kupinga, wanajiepusha nao (huo ubatilifu na ulaghai) na hawauridhii kwa wengine.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net