Al-Furqaan 25:71
الفرقانوَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَـٰلِحًا فَإِنَّهُۥ يَتُوبُ إِلَى ٱللَّهِ مَتَابًا
Na aliyetubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na aliye tubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu. [71]
[71] Na hivyo ndio mambo yetu yendavyo, yaani kuwa mwenye kutubu madhambi, na akaonyesha matokeo yake katika kukubali ut'iifu na kuepuka maasi, basi huyo Mwenyezi Mungu huikubalia toba yake. Na kwa hivyo hurejea kwa Mola wake Mlezi baada ya kumwacha kwake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na yoyote anayetubia kwa madhambi aliyoyafanya na akafanya matendo mema, basi yeye, kwa hilo, atakuwa amerudi kwa Allah Mtukufu kisawasawa, na hapo Allah Mtukufu Ataikubali toba yake na Atazifuta dhambi zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net