Al-Furqaan 25:70
الفرقانإِلَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَـٰلِحًا فَأُو۟لَـٰٓئِكَ يُبَدِّلُ ٱللَّهُ سَيِّـَٔاتِهِمْ حَسَنَـٰتٍ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا
Isipokuwa atakayetubu, na akaamini, na akatenda matendo mema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [70]
[70] Lakini mwenye kutubu na madhambi haya na akawa mkweli katika Imani yake, na akafuatiliza hayo kwa ut'iifu na vitendo vyema, hao atawasamehe kwa rehema yake, na atawajaalia bora ya thawabu badala ya maovu yaliyo kwisha tangulia. Na hakika shani ya Mwenyezi Mungu ni kurehemu na kusamehe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lakini mwenye kutubia kutokana na madhambi haya toba ya dhati, na akaamini imani ya kukata yenye kuambatana na matendo mema, basi hao Allah Mtukufu Atawafutia makosa yao na Atawaweka mahali Pake pema, kwa sababu ya kutubia kwao na kujuta kwao. Na kwa hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia, ni Mwingi wa rehema kwa waja Wake, kwa kuwa Amewaita watubie baada ya kushindana na Yeye kwa kufanya maasia makubwa kabisa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net