Al-Furqaan 25:69
الفرقانيُضَـٰعَفْ لَهُ ٱلْعَذَابُ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِۦ مُهَانًا
Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheshwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka. [69]
[69] Na Siku ya Kiyama atapata adhabu mardufu kuliko hiyo, na atadumu Motoni kwa udhalili na unyonge.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ataongezewa adhabu maradufu Siku ya Kiyama na atakaa humo milele akiwa mdhalilifu mnyonge. Onyo la kukaa milele ni kwa wale wanaoyafanya yote hayo au ni kwa yule aliyemshirikisha Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net