Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 68

Al-Furqaan 25:68

الفرقان

وَٱلَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ ٱلنَّفْسَ ٱلَّتِى حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا

Maana

Na wale wasiomuomba mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyoiharimisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, wala hawazini. Na atakayefanya hayo, atapata madhara.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara, [68]

[68] Na katika sifa zao hao waja wa Mwenyezi Mungu ni kuwa wameisafia niya Tawhid, na wakatupilia mbali kila athari ya ushirikina katika kumuabudu Mola wao Mlezi. Na wakajizuia kuuwa nafsi aliyo kataza Mwenyezi Mungu kuuliwa, ila ikiwa imefanya uadui basi huuliwa kwa haki. Nao hujitenga mbali na uzinzi, na katika mambo ya starehe hawatendi ila lilio halali tu, ili waepukane na adhabu ya mambo yanayo angamiza. Kwani anaye tenda katika mambo hayo atakuta shari na adhabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ambao wanampwekesha Allah Mtukufu na hawamuombi wala kumuabudu mola asiyekuwa Yeye, wala hawaiui nafsi ambayo Allah Mtukufu Ameharamisha kuuawa isipokuwa kwa kitu kinachopasisha kuuawa, kama vile kukufuru baada ya kuamini, au kuzini baada ya ndoa, au kumuua mtu kwa uadui, wala hawazini, bali wanazihifadhi tupu zao isipokuwa kwa wake zao au wale ambao mikono yao ya kulia imemiliki. Na mwenye kuyafanya madhambi haya makubwa atakuta mateso huko Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net