Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 32

An-Noor 24:32

النور

وَأَنكِحُوا۟ ٱلْأَيَـٰمَىٰ مِنكُمْ وَٱلصَّـٰلِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَآئِكُمْ ۚ إِن يَكُونُوا۟ فُقَرَآءَ يُغْنِهِمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ

Maana

Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua. [32]

[32] Na saidieni katika kujitenga na zina na yanayo pelekea zina, kwa kuwaoza ambao bado hawajaoana miongoni mwa wanaume wenu na wanawake wenu, na walio kuwa wanafaa kwa hayo katika watumwa wenu. Na wala umasikini usiwe sababu ya kuzuilia kuoa. Kwani Mwenyezi Mungu atasahilisha njia za maisha mazuri kwa mwenye kutaka kuishi maisha safi. Na fadhila za Mwenyezi Mungu ni kunjufu, na Yeye anajua kabisa niya za watu, na kila lipitalo katika ulimwengu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na waozeni, enyi Waumini, wanaume wasiokuwa na wake na wanawake wasiokuwa na waume, miongoni mwa waungwana na walio wema kati ya watumwa wenu na wajakazi wenu. Iwapo anayetaka kuoa kwa kujihifadhi ni masikini mwenye uhitaji, Allah Mtukufu Atamtosheleza kutokana na ukunjufu wa riziki Yake. Na Allah Mtukufu ni Mkunjufu, ni Mwingi wa kheri, ni Mkuu wa fadhila na ni Mjuzi mno wa nyenendo za waja Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net