Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 31

An-Noor 24:31

النور

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَـٰتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَـٰرِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ ءَابَآئِهِنَّ أَوْ ءَابَآءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَآئِهِنَّ أَوْ أَبْنَآءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَٰنِهِنَّ أَوْ بَنِىٓ إِخْوَٰنِهِنَّ أَوْ بَنِىٓ أَخَوَٰتِهِنَّ أَوْ نِسَآئِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُهُنَّ أَوِ ٱلتَّـٰبِعِينَ غَيْرِ أُو۟لِى ٱلْإِرْبَةِ مِنَ ٱلرِّجَالِ أَوِ ٱلطِّفْلِ ٱلَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا۟ عَلَىٰ عَوْرَٰتِ ٱلنِّسَآءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَ ٱلْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Maana

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume zao, au watoto wao wa kiume, au watoto wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyowamiliki mikono yao ya kiume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yanayohusu uchi wa wanawake. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyoyaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa. [31]

[31] Vile vile ewe Nabii, waambie wanawake Waumini, wanaamrishwa waache kutazama yaliyo harimishwa, na wazihifadhi tupu zao kwa kuzisitiri na kutoingiliwa ila kwa njia ya Kisharia. Na wasiwaonyeshe wanaume ya kuwavutia katika uzuri wa umbo lao na mapambo, kama kifua, mabega, vidani, isipo kuwa yale tangu hapo yamedhihiri, kama uso na mikono. Na ewe Nabii! Watake hao wanawake wajisitiri mwahali zilipo funuka nguo, kama shingo na kifua. Na hayo kwa kuteremshia vitambaa vya kichwani. Na wasiachilie kuonekana uzuri wao ila kwa waume zao, na jamaa ambao ni haramu kuoana nao milele, kama baba zao, au baba za waume wao, au watoto wao, au watoto wa waume zao kwa wake wengine, au kaka zao, au watoto wa kaka zao, au watoto wa dada zao. Na mfano wa hawa ni wanawake wenzao, sawa sawa wakiwa waungwana au wajakazi, na wanaume wanao ishi nao na hawana tena haja ya wanawake kwa ukongwe. Na kadhaalika watoto wadogo ambao hawajafikilia miaka ya kutamani. Na pia watake wanawake wasifanye vituko vya kutaka kuwavutia wanaume kama kugonga miguu chini ili isikilizane milio ya mitali na kugesi iliyo fichikana ndani ya nguo. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, kwa mlivyo iacha amri ya Mwenyezi Mungu. Na shikamaneni na adabu za Dini mpate kuongokewa katika dunia na Akhera yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na useme kuwaambia Waumini wanawake wayainamishe macho yao kutoyaangalia yasiokuwa halali kwao miongoni mwa tupu, na wazilinde tupu zao na yale Aliyoyaharamisha Allah Mtukufu, wala wasionyeshe waziwazi pambo lao kwa wanaume, bali wajipinde kulificha pambo lao isipokuwa nguo za juu ambazo imezoeleka kuzivaa, iwapo hakuna kwenye nguo hizo kivutio cha kupelekea kufitinika nao, na waviangushe vifiniko vya vichwa vyao kwenye uwazi wa sehemu za juu za nguo zao kwenye sehemu za vifua vyao huku wamezifunika nyuso zao ili sitara yao itimie. Na wasiuonyeshe urembo uliofichika isipokuwa kwa waume zao, kwani wao wanaona kutoka kwao wasiyoyaona wengine. Na sehemu ya urembo huo, kama uso, shingo, mikono miwili na sehemu za begani za mikono, zinafaa kuonekana na baba zao au baba za waume zao au watoto wao au watoto wa waume zao au ndugu zao au watoto wa ndugu zao wa kiume, au watoto wa dada zao au wanawake wenzao, walio Waislamu na sio makafiri, au watumwa waliowatawala au wafuasi kati ya wanaume ambao hawana malengo wala haja ya wanawake, kama vile mapite wanaowafuata watu kwa sababu ya kula au kunywa tu, au watoto wadogo ambao hawana ujuzi wowote wa mambo yanayohusiana na tupu za wanawake na ambao bado hawana matamanio. Na wasipige miguu yao, hao wanawake, wanapotembea ili kuwasikilizisha watu mapambo yao yaliyofichika, kama vikuku (vinavyovaliwa kama pambo) na mfano wake. Na rudini, enyi Waumini, kwenye kumtii Allah Mtukufu katika yale Aliyowaamrisha kwayo kati ya sifa hizi nzuri na tabia njema, na yaacheni yale ambayo walikuwa nayo watu wa zama za ujinga ya tabia na sifa mbovu kwa matarajio mfaulu kuzipata kheri mbili: ya ulimwenguni na ya Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net