An-Noor 24:30
النورقُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا۟ مِنْ أَبْصَـٰرِهِمْ وَيَحْفَظُوا۟ فُرُوجَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَزْكَىٰ لَهُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرٌۢ بِمَا يَصْنَعُونَ
Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za wanayoyafanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za wanayo yafanya. [30]
[30] Ewe Nabii! Waambie Waumini katika yanayo pelekea zina na kutilisha shaka, wasitazame yanayo harimishwa kutazama, nayo ni tupu za wanawake na sehemu za uzuri wao, na wanaume wahifadhi tupu zao kwa kuzisitiri na kuto zitumilia kwa njia isiyo ruhusiwa na Sharia. Adabu hiyo ndio ina hishima zaidi na safi zaidi kwao wasiingie katika maasi na tuhuma. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua baraabara yote wayatendayo, na atakuja walipa kwayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Nabii, uwaambie Waumini wanaume wayainamishe macho yao kutoangalia vitu visivyohalali kwao miongoni mwa wanawake na tupu, na wazilinde tupu zao na vile Alivyovifanya haramu Allah Mtukufu miongoni mwa uzinifu, ulawiti, kufunua tupu na mfano wa hayo. Kufanya hivyo ni usafi zaidi kwao. Kwa hakika, Allah Mtukufu ni Mtambuzi wa wanayoyafanya katika yale Anayowaamrisha na kuwakataza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net