Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 29

An-Noor 24:29

النور

لَّيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَدْخُلُوا۟ بُيُوتًا غَيْرَ مَسْكُونَةٍ فِيهَا مَتَـٰعٌ لَّكُمْ ۚ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ

Maana

Si vibaya kwenu kuingia nyumba zisiokaliwa ambazo ndani yake yamo manufaa yenu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnayoyadhihirisha na mnayoyaficha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Si vibaya kwenu kuingia nyumba zisio kaliwa ambazo ndani yake yamo manufaa yenu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnayo yadhihirisha na mnayo yaficha. [29]

[29] Na mkitaka kuingia nyumba za umma zisio kaliwa na watu makhsusi na ndani yake zipo haja zenu, kama vile maduka, mahoteli, nyumba za ibada, hapana ubaya kuingia bila ya kutaka ruhusa. Na Mwenyezi Mungu anajua kwa ujuzi wa timamu kabisa vitendo vyenu vyote vya dhaahiri na vilivyo fichikana. Basi tahadharini na kwenda kinyume naye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lakini hapana ubaya kwenu kuingia, bila ya kubisha hodi, nyumba ambazo hazikuwekwa kuwa ni makazi ya watu maalumu wajulikanao isipokuwa ziwe ni maliwazo kwa wenye kuzihitajia, kama nyumba zilizowekwa kuwa ni sadaka kwa mpita njia kwenye njia ya wasafiri, na zisokuwa hizo katika huduma. Basi ndani ya nyumba hizo muna manufaa na mahitaji ya wenye kuyaingia, kwani kubisha kwenye hali hiyo ni usumbufu. Na Allah Mtukufu Anazijua hali zenu zilizo waziwazi na za zilizofichika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net