Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 33

An-Noor 24:33

النور

وَلْيَسْتَعْفِفِ ٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ ۗ وَٱلَّذِينَ يَبْتَغُونَ ٱلْكِتَـٰبَ مِمَّا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُكُمْ فَكَاتِبُوهُمْ إِنْ عَلِمْتُمْ فِيهِمْ خَيْرًا ۖ وَءَاتُوهُم مِّن مَّالِ ٱللَّهِ ٱلَّذِىٓ ءَاتَىٰكُمْ ۚ وَلَا تُكْرِهُوا۟ فَتَيَـٰتِكُمْ عَلَى ٱلْبِغَآءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِّتَبْتَغُوا۟ عَرَضَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۚ وَمَن يُكْرِههُّنَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ مِنۢ بَعْدِ إِكْرَٰهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Na wajizuilie mbali na machafu wale wasiopata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe kwa fadhila yake. Na wanaotaka kuandikiwa uhuru katika wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikieni kama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyowapa. Wala msiwashurutishe vijakazi vyenu kufanya zina kwa ajili ya kutafuta pato la maisha ya dunia, ilhali wao wanataka kujiheshimu. Na atakayewalazimisha basi Mwenyezi Mungu baada ya kulazimishwa kwao huko, atawasamehe, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wajizuilie na machafu wale wasio pata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe kwa fadhila yake. Na wanao taka kuandikiwa uhuru katika wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikieni kama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyo kupeni. Wala msiwashurutishe vijakazi vyenu kufanya zina kwa ajili ya kutafuta pato la maisha ya dunia, ilhali wao wanataka kujihishimu. Na atakaye walazimisha basi Mwenyezi Mungu baada ya kulazimishwa kwao huko, atawasamehe, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [33]

[33] Na ambao hawakupata uwezo wa fedha za kuolea basi wafuate mojapo wa njia nyengine kama saumu na riyadha na kazi za kutumia akili . Kwa hayo hujikurupusha mpaka Mwenyezi Mungu akawafungulia kwa fadhila zake zitakazo wawezesha kuoa. Na watumwa ambao wanataka kuandikiana nanyi ili wapate uhuru wao ni waajibu juu yenu kuwakubalia walitakalo, mkijua kuwa watatimiza kutekeleza na wanaweza. Na juu yenu kuwasaidia waweze kutimiza walio andikiana nanyi, na hayo ama ni kwa kuwapunguzia shuruti mlizo andikiana nao, au kwa kuwapa mali katika mali aliyo kuneemesheni Mwenyezi Mungu, mkawapa katika Zaka au Sadaka. Na ni haramu juu yenu kuwafanya vijakazi vyenu njia ya pato la duniani rakhisi kwa kuwafanya makahaba, na mkawalazimisha kwa hayo. Na vipi mnakwenda kumlazimisha uchafu anaye taka kuwa safi? Na mwenye kuwalazimisha, basi Mwenyezi Mungu humsamehe mwenye kulazimisha pindi akitubu kwa dhambi zake za kulazimisha. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa maghfira na rehema. Haya yanaelezwa na kauli ya Mtume s.a.w.: "Enyi vijana! mwenye kuweza kuwoa na aoe kwani hivyo linalindwa jicho, unahifadhiwa utupu. Asiye weza na afunge, kwani hivyo ni kinga yake."

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale wasiokuwa na uwezo wa kuoa kwa ufukara wao au kwa jambo lingine, basi na wajizoeze uvumilivu wa kutoyafanya Aliyoyakataza Allah Mtukufu, mpaka Allah Mtukufu Awatosheleze kwa wema Wake na Awasahilishie kuoa. Na wale wanaotaka kujikomboa na utumwa na ujakazi kwa kufanya mkataba na mabwana zao kwa kutoa kiasi maalumu cha pesa wawapatie, basi ni juu ya hao wamiliki wao waandikiane mapatano na wao kwa hilo, iwapo watajua kuwa kuna wema ndani yao ya uongofu, uwezo wa kujitafutia pesa na wema wa Dini. Na ni juu yao, hao wamiliki, wawape pesa, hao watumwa wao, au wawasamehe sehemu ya pesa walioandikiana. Na haifai kwenu kuwalazimisha wajakazi wenu kufanya uzinifu kwa lengo la kutaka kupata pesa. Na vipi litapatikana kwenu hilo na huku wao wenyewe wanataka kujilinda na uchafu huo, na nyinyi mnawakatalia hilo? Katika haya, pana kuonesha ubaya wa kitendo kiovu walichokifanya. Na yoyote mwenye kuwalazimisha wao kufanya uzinifu, basi Allah Mtukufu Aliyetukuka, baada ya kuwalazimisha wao, ni mwenye kuwasamehe (hao waliolazimishwa) na kuwaonea huruma, na dhambi ni kwa yule Aliyewalazimisha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net