Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 34

An-Noor 24:34

النور

وَلَقَدْ أَنزَلْنَآ إِلَيْكُمْ ءَايَـٰتٍ مُّبَيِّنَـٰتٍ وَمَثَلًا مِّنَ ٱلَّذِينَ خَلَوْا۟ مِن قَبْلِكُمْ وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ

Maana

Na kwa yakini tumewateremshia Ishara zilizo wazi, na mifano kutokana na waliotangulia kabla yenu na mawaidha kwa wacha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kwa yakini tumekuteremshieni Ishara zilizo wazi na mifano kutokana na walio tangulia kabla yenu na mawaidha kwa wachamngu. [34]

[34] Na Sisi tumekuteremshieni katika Sura hii na nyenginezo Aya zilizo wazi zenye kubainisha hukumu. Na tumekuteremshieni mifano ya hali mbali mbali za walio tangulia, na uwongozi, na mawaidha ambayo kwayo watapata faida wenye kumkhofu Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika tumewateremshia, enyi watu, aya za Qur’ani zikiwa ni dalili za wazi za kuonesha haki, na ni mfano wa matukio ya ummah uliopita wa Waumini kati yao na makafiri, na yaliyowapitia ya kuwafaa na kuwadhuru ambayo ni mfano na mazingatio kwenu, na ni mawaidha ya kuwaidhika mwenye kumcha Allah Mtukufu na kujihadhari na adhabu Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net