Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 2

An-Noor 24:2

النور

ٱلزَّانِيَةُ وَٱلزَّانِى فَٱجْلِدُوا۟ كُلَّ وَٰحِدٍ مِّنْهُمَا مِا۟ئَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِى دِينِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۖ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَآئِفَةٌ مِّنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isiwashike huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini. [2]

[2] Na miongoni mwa hukumu hizo ni hukumu ya mwanamke na mwanamume wenye kuzini. Basi kila mmoja wao mpigeni fimbo mia. Wala huruma kwao isikuzuieni kutimiza hukumu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Kwani yanayo takikana na Imani ni kukhiari kumridhi Mwenyezi Mungu kuliko kuwaridhi watu. Na wahudhurie baadhi ya jamaa Waumini waone hiyo adhabu inavyo tekelezwa, ili adhabu hiyo iwatishe wenginewe wasitende hivyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mzinifu mwanamume na mzinifu mwanamke ambao hawajawahi kuoa au kuolewa, adabu ya kila mmoja kati yao ni kupigwa mboko mia moja. Na imethibiti katika Sunnah (mapokezi kutoka kwa Mtume) kwamba pamoja na mboko hizi, ahamishwe kwa kipindi cha mwaka mmoja. Wala kusiwafanye nyinyi kule kuwahurumia kuacha kuwatia adabu hiyo au kuipunguza, iwapo mnamuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho na mnazifuata kivitendo hukumu za Kiislamu. Na waihudhurie adabu hiyo kikundi cha Waumini kwa kuwaumbua na iwe ni onyo, mawaidha na mazingatio.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net