Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Noor
Sura ya 24

An-Noor

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 2

ٱلزَّانِيَةُ وَٱلزَّانِى فَٱجْلِدُوا۟ كُلَّ وَٰحِدٍ مِّنْهُمَا مِا۟ئَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِى دِينِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۖ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَآئِفَةٌ مِّنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ 2

Kisha akaendelea kubainisha hukumu hizo zilizoashiriwa juu yake, akasema:

{2} Hukumu hii ni kwa mzinifu mwanamume na mzinifu mwanamke ambao ni mabikira. Kwamba hao wawili watapigwa mijeledi mia kila mmoja. Ama yule ambaye si bikira, basi hakika imejulisha Sunnah sahihi inayojulikana sana kwamba adhabu yake ni kupigwa mawe hadi kufa. Ametukataza Mwenyezi Mungu aliyetukuka kuwahurumia katika dini ya Mwenyezi Mungu, ambapo huruma huo utatuzuia kusimamisha adhabu juu yao hao wawili, sawa iwe ni huruma ya kimaumbile, au kwa ajili ya ukoo, urafiki, au mengineyo, na kwamba imani inalazimu kutokuwepo huruma hii inayotuzuia kutekeleza agizo la Mwenyezi Mungu. Basi hakika rehema yake ni katika kusimamisha adhabu juu yake. Basi sisi hata tukimrehemu katika kupitiwa na qadari juu yake, basi tusingemrehemu katika upande huu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akaamrisha kwamba adhabu ya wazinifu ihudhuriwe na "kundi." Yaani, kundi la waumini, ili awe maarufu kwa adhabu aliyopewa na apate kutokana na hilo fedheha na kurudi nyuma katika kosa hilo. Na washuhudie adhabu hiyo kwa vitendo, kwani hakika kushuhudia hukumu za kisheria kwa vitendo ndiko kunakoimarisha elimu, kuleta utulivu wa ufahamu, na kumleta mtu kuwa karibu na kupata ukweli. Haiongezeki ndani yake wala haipungui. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.