An-Noor 24:1
النورسُورَةٌ أَنزَلْنَـٰهَا وَفَرَضْنَـٰهَا وَأَنزَلْنَا فِيهَآ ءَايَـٰتٍۭ بَيِّنَـٰتٍ لَّعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
Hii ni Sura tuliyoiteremsha na tukailazimisha; na tukateremsha ndani yake Aya zilizo wazi ili mkumbuke.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
HII NI SURA Tuliyo iteremsha na tukailazimisha; tukateremsha ndani yake Aya zilizo wazi ili mkumbuke. [1]
[1] Sura hii tumeifunua na tumewajibisha hukumu zake, na tumeteremsha ndani yake dalili zilizo wazi za kuthibitisha uwezo wa Mwenyezi Mungu na upweke wake, na kwamba Kitabu hichi kinatoka kwake, ili mpate kuwaidhika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hii ni sura kubwa miongoni mwa sura za Qur’ani, tumeiteremsha na tumelazimisha kuzifanyia kazi hukumu zake, na tumeteremsha ndani yake hoja nyingi zilizo waziwazi ili mpate kujikumbusha, enyi Waumini, kwa aya hizi zilizo waziwazi na mzifanyie kazi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net