Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 3

An-Noor 24:3

النور

ٱلزَّانِى لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَٱلزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَآ إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Mwanamume mzinifu hamwoi ila mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina. Na hayo yameharamishwa kwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina. Na hayo ya. Mwanamume mzinifu hamwoi ila mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke meharimishwa kwa Waumini. [3]

[3] Mwanamume muovu aliye zoea uzinifu hapendi kumwoa ila mchafu anaye zini au mshirikina. Na mwanamke mchafu ambaye kazi yake ni uzinifu hapendelei kuolewa ila na mchafu anaye zini;au mshirikina. Na ndoa namna hii haiwaelekei Waumini, kwa kuwa imeshabihi fiski na kupelekea kutuhumiwa. Haya ikiwa haikupita toba. Na tafsiri ya haya ni kuwa inabainishwa tabia za washirikina au wazinifu kuwa wao hawapendi ila mambo ya ufisadi tu. Na kwa mujibu wa maoni ya Hambali na Ahli-Dhaahir (na pia Ibadhi) haisihi ndoa ya mwanamume mzinifu au mwanamke mzinifu kabla ya toba.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mwanamume mzinifu haridhiki isipokuwa kumuoa mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina asiyekubali uharamu wa uhalifu wa uzinifu, na mwanamke mzinifu haridhiki isipokuwa kuolewa na mwanamume mzinifu au mwanaume mshirikina asiyekubali uharamu wa uzinifu. Ama wanaume na wanawake wanaojizuia na uzinifu, wao hawaridhiki na hilo, na ndoa hiyo imeharamishwa kwa Waumini. Na huu ni ushahidi wazi wa uharamu wa kumuoa mwanamke mzinifu mpaka atubie, vilevile uharamu wa kumuoza mwanamume mzinifu mpaka atubie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net