Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 8

Al-Muminoon 23:8

المؤمنون

وَٱلَّذِينَ هُمْ لِأَمَـٰنَـٰتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَٰعُونَ

Maana

Na ambao wanazitunza amana zao na maagano yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao! [8]

[8] Na (hao Waumini) wawe ni wenye kuhifadhi kila walicho pewa kuwa ni amana, ikiwa mali au neno au kitendo au chenginecho, na watimize kila ahadi iliyo baina yao na Mwenyezi Mungu au na watu. Wasikhuni amana, wala wasivunje ahadi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale ambao wanavitunza vitu vyote walivyoaminiwa navyo na wanatekeleza ahadi zao zote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net