Al-Muminoon 23:7
المؤمنونفَمَنِ ٱبْتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْعَادُونَ
Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio wavukao mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka. [7]
[7] Mwenye kutaka kuingiliana na mwanamke bila ya kupitia njia hizi mbili, basi huyo amevuka mipaka ya sharia hadi ya kuvuka. Na (hao Waumini) wawe ni wenye kuhifadhi kila walicho pewa kuwa ni amana, ikiwa mali au neno au kitendo au chenginecho, na watimize kila ahadi iliyo baina yao na Mwenyezi Mungu au na watu. Wasikhuni amana, wala wasivunje ahadi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi mwenye kutaka kujistarehesha na asiyekuwa mkewe au mjakazi wake, huyo ni miongoni mwa wenye kuikiuka halali na kuijia haramu na atakuwa amejiorodhesha nafsi yake kwenye mateso ya Allah Mtukufu na hasira Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net