Al-Muminoon 23:6
المؤمنونإِلَّا عَلَىٰٓ أَزْوَٰجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ
Isipokuwa kwa wake zao au kwa wale iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. [6]
[6] Isipo kuwa kwa njia ya ndoa ya kisharia, au wenye kumiliki masuria. Hao hawalaumiwi. Zamani utumwa ulikuwa ni jambo la kawaida, na ilikuwa mtu akiweza kuchukua katika wajakazi wake akawafanya kuwa ni wakeze. Na Uislamu ulihalalisha utumwa wa mateka katika vita vilivyo fuata sharia ikiwa maadui nao wanakamata watumwa, basi ilikuwa ni halali kuwatendea wao hali kadhaalika. Ikiwa maadui hawawafanyi mateka kuwa ni watumwa basi ilikuwa haiwafalii Waislamu kuwafanya mateka kuwa ni watumwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Isipokuwa kwa wake zao au wajakazi waliomilikiwa na mikono yao ya kulia. Hao, Waumini hawana lawama wala makosa kuwaingilia na kujistarehesha nao, kwa kuwa Allah Mtukufu Amewahalalishia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net