Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 76

Al-Muminoon 23:76

المؤمنون

وَلَقَدْ أَخَذْنَـٰهُم بِٱلْعَذَابِ فَمَا ٱسْتَكَانُوا۟ لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ

Maana

Na hakika tuliwatia adhabu kali; lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi wala hawakunyenyekea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika tuliwatia adhabu kali; lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi wala hawakunyenyekea. [76]

[76] Na Sisi kwa hakika tuliwapa adhabu kama kwa kuwauwa au kuwaletea njaa. Na wala hawakumnyenyekea Mola wao Mlezi, bali waliendelea na jeuri zao na kiburi chao kiasi ya kuondoka tu hiyo adhabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika, tuliwajaribu wao kwa kuwaonja kwa aina mbalimbali za mikasa, pamoja na hivyo wasimnyenyekee Mola wao na wasimuombe kwa unyenyekevu wakati wa kushukiwa na hiyo mikasa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net