Al-Muminoon 23:75
المؤمنونوَلَوْ رَحِمْنَـٰهُمْ وَكَشَفْنَا مَا بِهِم مِّن ضُرٍّ لَّلَجُّوا۟ فِى طُغْيَـٰنِهِمْ يَعْمَهُونَ
Na lau tungeliwarehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo, bila ya shaka wangeliendelea katika upotovu wao, vile vile wakitangatanga.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau tungeli warehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo bila ya shaka wangeli endelea katika upotofu wao vile vile, wakitangatanga. [75]
[75] Na lau tungeli warehemu, na tukawaondolea madhara yalio wateremkia katika miili yao, na ukame katika mali yao, na mfano wa hayo, basi hapana shaka yoyote wangeli zidi ukafiri, na wakaendelea katika maasi na jeuri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau tungewahurumia na tukawaaondolea ukame na njaa, wangeendelea kwenye ukafiri na ushindani, wakiwa katika hali ya kuduwaa na kukosa muelekeo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net