Al-Muminoon 23:74
المؤمنونوَإِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ عَنِ ٱلصِّرَٰطِ لَنَـٰكِبُونَ
Na hakika wale wasioiamini Akhera wanajitenga mbali na njia hiyo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika wale wasio iamini Akhera wanajitenga na Njia hiyo. [74]
[74] Na hakika hao wasio iamini Akhera na yalioko huko ya Pepo au Moto wanaiacha Njia Iliyo Nyooka inayo mhifadhi mpitaji wakaishika njia ya ubabaishi na misukosuko na ufisadi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika, wale ambao hawaamini kufufuliwa na kuhesabiwa wala hawayafanyii kazi hayo mawili, basi hao wamepotoka kando ya njia ya Dini iliyonyooka, nayo ni dini ya Uislamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net