Al-Muminoon 23:77
المؤمنونحَتَّىٰٓ إِذَا فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا ذَا عَذَابٍ شَدِيدٍ إِذَا هُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ
Mpaka tulipowafungulia mlango wa adhabu, hapo ndipo wakawa wenye kukata tamaa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mpaka tulipo wafungulia mlango wa adhabu kali, hapo ndipo wakawa wenye kukata tamaa. [77]
[77] Wanashikilia kupuuza kwao mpaka pale tunapo wapatiliza kwa adhabu kali ya njaa au mauwaji hapa duniani huwa tena wanababaika na kukata tamaa, hawaioni njia ya kuvuka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mpaka tulipowafungulia juu yao mlango wa adhabu kali huko Akhera, wakitahamaki wamo ndani yake, wamekata tamaa kupata kheri yoyote, wamechanganyikiwa hawajui wafanye nini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net