Al-Muminoon 23:78
المؤمنونوَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنشَأَ لَكُمُ ٱلسَّمْعَ وَٱلْأَبْصَـٰرَ وَٱلْأَفْـِٔدَةَ ۚ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ
Na Yeye ndiye aliyewaumbia kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu. Ni kuchache mno kushukuru kwenu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Yeye ndiye aliye kuumbieni kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu. Ni kuchache mno kushukuru kwenu. [78]
[78] Na yawaje mkamkufuri Mwenyezi Mungu na hali ni Yeye ndiye aliye kuumbieni usikizi mkaisikia Haki, aliye kupena uwezo wa kuona mkauona ulimwengu na viliomo ndani yake, na akakupeni akili mzingatie kwayo utukufu wake mpate kuamini? Hakika nyinyi hamumshukuru Mwenye kuumba vyote hivyo kwa Imani na ut'iifu ila kwa uchache tu, nao ni uchache mno!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na yeye Ndiye Aliyewaumbia masikio ya kuvisikia vyenye kusikika, na macho ya kuviona vyenye kuonekana, na nyoyo ili muelewe. Pamoja na hayo, shukrani zenu kwa hizi neema za mfululizo juu yenu bado ni chache hata hazitajiki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net