Al-Hajj 22:7
الحجوَأَنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَأَنَّ ٱللَّهَ يَبْعَثُ مَن فِى ٱلْقُبُورِ
Na kwamba hakika Saa (ya Kiyama) itakuja hakuna shaka kwa hilo, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwamba hakika Saa (Kiyama) itakuja hapana shaka kwa hilo, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini. [7]
[7] Hayo yaliyo tangulia ya kuumbwa binaadamu, na mimea ya kupanda, ni ushahidi ya kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mungu wa Haki. Na kwamba hakika Yeye ndiye anaye huisha maiti wakati wa kufufuliwa kama vile alivyo anza kuwaumba. Na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu, na kwamba hakika Kiyama kinakuja tu bila ya shaka kuhakikisha ahadi yake. Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawahuisha waliomo makaburini kwa kuwafufua kwa ajili ya hisabu na malipo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwamba wakati wa ufufuzi ni wenye kuja, hilo halina shaka, na kwamba Allah Mtukufu Atawafufua wafu kutoka makaburini mwao ili Awahesabu na Awalipe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net