Al-Hajj 22:6
الحجذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْحَقُّ وَأَنَّهُۥ يُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَأَنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Hayo ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki, na kwamba hakika Yeye ndiye mwenye kuhuisha wafu, na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hayo ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki, na kwamba hakika Yeye ndiye mwenye kuhuisha wafu, na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu. [6]
[6] Hayo yaliyo tangulia ya kuumbwa binaadamu, na mimea ya kupanda, ni ushahidi ya kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mungu wa Haki. Na kwamba hakika Yeye ndiye anaye huisha maiti wakati wa kufufuliwa kama vile alivyo anza kuwaumba. Na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu, na kwamba hakika Kiyama kinakuja tu bila ya shaka kuhakikisha ahadi yake. Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawahuisha waliomo makaburini kwa kuwafufua kwa ajili ya hisabu na malipo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hayo yaliyotangulia kutajwa, miongoni mwa alama za uwezo wa Allah Mtukufu Aliyetukuka, ndani yake pana dalili ya kukata kwamba Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kutakasika, Ndiye Mola Mwenye kuabudiwa kwa haki Ambaye hakuna anayefaa kuabudiwa isipokuwa Yeye, na Yeye Ndiye Mwenye kuwahuisha wafu, na Yeye ni Muweza wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net